BAJETI 2024/25 TRILIONI 49.3
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwenye Kamati ya Bunge zima, jijini Dodoma.
Serikali imepanga kukusanya na kutumia Sh trilioni 49.34 kwa mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24 ya Sh trilioni 44.39.
Hayo yamesemwa leo Machi 11,2024 na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mfumo na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwenye Kamati ya Bunge zima, jijini Dodoma.
Amesema mapato yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni Sh trilioni 29.8 wakati mapato yasiyo ya kodi ni Sh trilioni 3.4 na mapato kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ni Sh trilioni 1.3.
Na Mwandishi Wetu, The Page