BABU DUNI AJITOA UENYEKITI ACT WAZALENDO
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji.
Saa chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu kama Babu Duni amejitoa kugombea nafasi hiyo.
Duni ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo kwa mara ya pili alikuwa akichuana na Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema Halmashauri Kuu ya Chama Taifa iliyokutana leo Machi 4,2024 imeridhia Duni kujitoa kugombea nafasi hiyo.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti Chama cha ACT Wazalendo, Juma Duni Haji (kulia), akipeana mkono na mpinzani wake, Othman Masoud Othman. Katikati ni Zitto Kabwe.
"Nimekabidhi rasmi barua yangu kwa Katibu wa Kamati Maalumu ya Uchaguzi Taifa na kuinakilisha barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa Chama na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uchaguzi Taifa - kwa taarifa na hatua zao, kuhusu kuondoa nia (kujitoa) kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa.
"Nimechukua uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 11(3) (7) na Ibara ya 76 (1) (p) na Ibara ya 111(3) zikisomwa pamoja, juu ya haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi, kazi na wajibu wa Halmashauri Kuu ya Chama kuwa ni "kujadili na kuidhinishwa na majina ya wagombea wa nafasi za Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama," amesema Duni.
Aidha amesema amefikia uamuzi huo kwa kuzingatia masilahi mapana ya chama, kuzingatia ushauri, maoni na mapendekezo ya viongozi wenzake na kuondoa taharuki iliyojitokeza.
Sababu nyingine ni kuimarisha umoja na maelewano miongoni mwao, kuelekeza nguvu zote dhidi ya washindani wao wa kisiasa, kutotoa nafasi ya mgawanyiko miongoni mwao na kumiachia Othman aendeleze mapambano ya kudai haki.
"Nimejiunga katika harakati za kudai haki na ukombozi kwa nchi zetu miaka 30 iliyopita ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nikiamini kuwa kufanya hivyo nitatoa mchango wangu katika kuwaunganisha Watanzania ili wakatae uonevu, kudhalilishwa, kunyanyaswa, kubaguliwa au maovu mengine yanayoweza kufanywa dhidi ya heshima ya utu wa binadamu, nitaendelea na msimamo huo," amesema Duni.
Na Nora Damian, Dar es Salaam