WALICHOTETA RAIS SAMIA, PAPA FRANCIS

Rais Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis jijini Vatican.

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jijini Vatican.

Katika mazungumzo yao wamejadili dhamira yao ya pamoja ya kuendelea kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Serikali na Kanisa Katoliki.

Aidha wamekubaliana pia kuendeleza juhudi za kuleta amani kidunia na kikanda, kupiga vita umaskini na mabadiliko ya tabia nchi na kukuza ustahimilivu wa kiimani.


Rais Samia pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin pamoja na Waziri anayeshughulikia masuala ya mahusiano na serikali mbalimbali katika Kuria ya Roma, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.

Askofu Mkuu Gallagher aliishi Tanzania miaka ya 1980 na anazungumza Kiswahili fasaha.



Powered by Blogger.