MAOFISA 155 WA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO WALA VIAPO
Aliyekuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Robert Mayala, ni miongoni mwa waliopandishwa vyeo na Rais Samia kuwa Naibu Kamishna wa Polisi.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Maofisa wa Jeshi la Polisi 155 waliopandishwa vyeo na Rais Samia Suluhu Hassan wamekula kiapo cha utii kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilius Wambura.
Maofisa hao wamekula kiapo pia cha maadili ya viongozi wa umma na kuahidi kupanda kwao vyeo kutakuwa chachu ya mabadiliko ya kiutendaji.
Waliokula kiapo ni makamishna wasaidizi waandamizi wa Polisi 27 waliopanda vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Polisi.
Wengine 128 wamekuwa makamishna wasaidizi wa Polisi waandamizi wa Polisi.
IGP Wambura amesema wananchi watarajie mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika Jeshi la Polisi.
