DK. NCHIMBI AKUMBUKA MAAMUZI MAGUMU YA LOWASSA
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, akitoa heshima kwa mwili wa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Lowassa, nyumbani kwake Ngarash Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Na Nora Damian, Monduli - Arusha
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emmanuel Nchimbi ametaja mambo matano watakayomkumbuka Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Lowassa akisema msiba huo ulikuwa ni habari mbaya kwake.
Dk. Nchimbi amesema Lowassa alikuwa mchapakazi, mwenye maamuzi magumu, mzalendo, mnyenyekevu na aliyependa watu wote bila kuwabagua.
Moja ya maamuzi magumu yanayoendelea kukumbukwa ni hatua ya kiongozi huyo kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 na ile ya kujiengua CCM na kujiunga Chadema mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 16,2024 nyumbani kwa Lowassa Kijiji cha Ngarash wilayani Monduli Mkoa wa Arusha, Dk. Nchimbi aliyetumia dakika mbili na sekunde 56 amesema kifo cha Lowassa ni pigo kubwa kwa nchi.
“Nilihisi kupoteza rafiki, kaka na mlezi lakini pia niliona jinsi ambavyo chama changu kimepoteza mtu. Niliona jinsi ambavyo nchi yetu imepoteza mtu, lakini niliona jinsi ambavyo vyama vingine vilivyokuwa karibu naye vimepoteza mtu muhimu sana kwao…pigo hili nililihisi binafsi na niliona ambavyo linaathiri nchi yetu, ni pigo kubwa sana kwa nchi yetu.
“Lowassa alikuwa Mwanaafrika wa kweli, alikuwa mtu wa maamuzi magumu na alikuwa mchapakazi, watu wanaweza wakapishana katika kila maelezo wanayotoa kuhusu Lowassa lakini hakuna hata mtu mmoja anayeweza kuwa na ujasiri wa kusema alikuwa mvivu au alikuwa hapendi kufanya kazi au hakuwa na mapenzi na nchi yake…alikuwa mchapakazi wa hali ya juu, hakupoteza muda hata mara moja kuacha kufanya kazi kwa ajili ya Watanzania,” amesema Dk. Nchimbi.
Amesema Lowassa alikuwa hachagui marafiki na wanajifunza kupitia kiongozi huyo kuishi maisha ya uadilifu, kuwa na marafiki wa aina zote na kuwatumikia watu wote bila ubaguzi.

“Alikuwa mnyenyekevu sana, nafasi alizozishika, aina ya marafiki aliokuwa nao, alikuwa na marafiki ambao haangalii nafasi zao, vyeo vyao na hata katika eneo hili tulilopo (nyumbani kwa Lowassa) wako watu wametoka mikoa mbalimbali nchini, watu wa kawaida kabisa ambao walikuwa marafiki wa Lowassa.
“Tunapopewa nafasi za uongozi lazima tuwapende tunaowatumikia hili ndilo jambo muhimu sana la kujifunza kutoka kwa Edward Lowassa.
“Nina ugonjwa wa kupenda watu wachapakazi, watu wa kweli, watu wanaoipenda nchi yao kwa dhati hayo yote ambayo mimi nayapenda Edward alikuwa nayo, haya ni mambo ya pekee ambayo nitamkumbuka.
“Ni mambo ambayo ningependa kuendelea kuyaenzi na kuwashawishi Watanzania wengine wayaenzi lakini mapenzi yake hayakuchagua aina ya itikadi ya mtu yeyote ndio maana alikuwa na marafiki CCM, Chadema, ACT vyama vyote vilikuwa ni marafiki zake,” amesema.

Lowassa alifariki Februari 10,2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa Februari 17,2024 nyumbani kwake Ngarash, Monduli mkoani Arusha.