WIZARA YA HABARI, JWTZ KUSHIRIKIANA SEKTA YA MAWASILIANO


Na Mwandishi Wetu


Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdullah ametoa wito kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kuendelea kushirikiana na wizara kwa lengo la kupata uelewa zaidi kuhusu majukumu na miradi inayotekelezwa.

Ameyasema hayo leo Januari 25, 2024 alipokutana na Kamati ya Wataalam wa Mawasiliano kutoka JWTZ waliofika ofisini kwake kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya mawasiliano.

Ameieleza kamati hiyo iliyooongozwa na Luteni Kanali Lukwaro Mbwambo kuwa wizara kupitia sekta ya mawasiliano ina miradi tisa ambayo inasimamia utekelezaji wake.



Amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Mkongo wa Taifa, mfumo wa anwani za makazi, mfumo wa jamii namba, usambazaji wa mawasiliano vijijini na ujenzi wa data center.

Miradi mingine ni kurusha Satelaiti, Chuo cha Tehama, kuendeleza bunifu katika Tehama pamoja na mafunzo kuhusu Teknolojia zinazoibukia katika tehama.

Akitoa salamu kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya JWTZ, Luteni Kanali Mbwambo ameishukuru wizara kwa wasilisho hilo na kuahidi kufanya uchambuzi ili kuona jeshi litakavyoweza kutumia miradi hiyo kujiimarisha katika eneo la mawasiliano.


 Abdullah ameteua timu ndogo ya wataalam itayoongozwa na maofisa waandamizi wa wizara ili kuungana na wataalam wa JWTZ na kuja na mapendekezo ya namna ya kuendelea na ushirikiano huo.
Powered by Blogger.