FCC KUADHIMISHA SIKU YA USHINDANI IKIWAFUNDA WADAU WAKE
Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani, Dar es Salaam.
Tume ya Ushindani (FCC) inatarajia kutoa mafunzo kwa wadau wake walioko katika kanda mbalimbali nchini ili wajiepushe na vitendo vinavyofifisha na kurudisha nyuma maendeleo.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani inayoadhimishwa Desemba 5 kila mwaka ambapo FCC inaungana na jumuiya nyingine za ushindani duniani katika kuiadhimisha.
Akizungumza leo Novemba 29,2023 wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo Mkurugenzi wa FCC, William Erio, amesema kutakuwa na wiki nzima ya kutoa elimu na semina mbalimbali kwa wananchi na wadau.
“Siku ya ushindani duniani ina lengo la kuelimisha wadau kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za biashara kuhakikisha utendaji wa biashara zote unakuwa halali na kuwa na usawa. Tunawasisitiza wafanyabiashara wafanye biashara kwa kuzingatia sheria na kanuni,” amesema Erio.
Na Nora Damian, Dar es Salaam

Amewataja wadau watakaonufaika na mafunzo hayo kuwa ni wachimbaji madini (Kanda ya Ziwa), wazalishaji na wasambazaji wa mbegu za maua (Kanda ya Kaskazini), wakamuaji wa mchuzi wa zabibu na mafuta ya alizeti (Kanda ya Kati), wafanyabiashara na wenye viwanda (Kanda ya Nyanda za Juu Kusini) na wakulima wa korosho.
Mkurugenzi huyo amewaomba wananchi na wadau hao kujitokeza kwa wingi kuhudhuria semina hizo na kusikiliza vipindi vitakavyokuwa vikirushwa katika redio mbalimbali nchini.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu ‘Njama baina ya washindani na madhara yake kwa wajali na watumiaji’ yatahitimishwa Desemba 5 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, atakuwa mgeni rasmi.