MHANDISI KEMIKIMBA AKABIDHI OFISI

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Profesa Jamal Katundu, akikabidhiwa ofisi na vitendea kazi kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

Mhandisi Kemikimba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini katika kipindi chote ambacho ameitumikia ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Aidha amemtakia majukumu mema Katibu Mkuu anayechukua nafasi yake na kuwataka watumishi kumuunga mkono kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuchapa kazi kwani Tanzania inamhitaji kila mmoja kwa nafasi na majukumu yake.

Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Wizara ya Maji wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Katibu Mkuu. Kutoka kushoto walioshika maua ni Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Mwajuma Waziri, Katibu Mkuu, Profesa Jamal Adam Katundu na aliyekuwa Katibu Mkuu, Mhandisi Nadhifa Kemikimba.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiagwa na aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba mara baada ya kukabidhi ofisi leo Septemba 4,2023 jijini Dodoma.

Powered by Blogger.