WANANCHI WAJENGEWA UWEZO MRADI WA MAJI MIJI 28


Na Mwandishi Wetu, Ruvuma


Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) na Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetembelea maeneo ambayo mradi wa Maji wa Miji 28 utatekelezwa ili kuwajengea uelewa wananchi.

Timu hiyo ya wataalamu imetembela na kukagua eneo ambalo mkandarasi amejenga kambi kwa ajili ya kuanza kutekeleza kazi hiyo.

Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) na unagharimu Sh bilioni 145.77.

Wananchi wamepokea kwa furaha kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na kuishukuru Serikali kwa kutenga fedha za ujenzi huo kwa kuwa utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Mji wa Songea.
Powered by Blogger.