PROFESA MKENDA ATAKA BUNIFU ZIINGIZWE SOKONI
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Veta, Anthony Kasore, akimuonesha Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda, mafuta na sabuni zinazotengenezwa kwa kutumia mawese na wahitimu wa vyuo hivyo baada ya kutembelea banda la mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Na Nora Damian, Mbeya
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza bunifu mbalimbali zinazovumbuliwa nchini ziendelezwe na kuingizwa sokoni ili ziweze kushindana katika soko la dunia.
Akizungumza Agosti 7, 2023 baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, amesema kuna maendeleo makubwa ya teknolojia yanayofanywa na taasisi mbalimbali za Serikali.
“Tumefurahishwa sana na bunifu ambazo tayari zimeanza kuingia sokoni, tunachohitaji vile vilivyogundulika visiwe tu vya maonesho mwaka huu au mwakani, tunataka tuvione vinaingia sokoni vinaanza kuuzwa.
“Veta tumeona vitu vingi vizuri, elimu ya utengenezaji simu, tumeona binti anayetengeneza simu ambaye amefundishwa na Veta…kwa ujumla banda lao ni zuri ningehimiza watu wapitie Veta kujifunza zaidi,” amesema Profesa Mkenda.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akizungumza na mhitimu wa Veta katika fani ya utengenezaji simu, Eunice Kavishe, kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Mmoja wa wahitimu wa Veta ambaye ni fundi simu, Eunive Kavishe, amesema kazi hiyo inamlipa na kuiomba Serikali kuendelea kuhamasisha vijana wengi zaidi kwenda kupata ujuzi Veta.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Veta, Anthony Kasore, amesema wanawafundisha vijana ili kuwaandaa kuingia kwenye soko la ajira katika nyanja mbalimbali za uwekezaji, viwanda, kilimo na ufugaji.
“Kwenye maonesho haya tumeonyesha wananchi kazi ambazo Veta tunazifanya ili kuhakikisha shughuli zinazotekelezwa za kiuchumi nchini zinapata usaidizi na kufanikishwa kwa haraka.
“Tumekuja na bunifu kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kufanya shughuli zao za kilimo na ufugaji kwa urahisi,” amesema Kasore.
Ametolea mfano utengenezaji wa vihenge vya chuma kudhibiti sumu kuvu, vifaa vinavyowasaidia wakulima kusaga bidhaa kwa urahisi, mashine ya kukaushia mazao na vyakula ili kuviongezea thamani na kumwezesha mkulima kuwa na bidhaa husika kwa muda mrefu bila kuharibika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akisalimiana na vijana waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza vihenge vya chuma kudhibiti sumu kuvu kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijjni Mbeya.
Kwa mujibu wa Kasore, kupitia mradi wa sumu kuvu vijana 420 kutoka katika wilaya 20 wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza vihenge ambapo Serikali itawapatia vifaa bure kuweza kujiajiri.
Kwa mujibu wa Kasore, kupitia mradi wa sumu kuvu vijana 420 kutoka katika wilaya 20 wamepatiwa ujuzi wa kutengeneza vihenge ambapo Serikali itawapatia vifaa bure kuweza kujiajiri.
Kaimu mkurugenzi huyo, amesema pia ujenzi wa vyuo vipya katika wilaya 64 na kimoja katika Mkoa wa Songwe utaongeza wigo wa mafunzo ya ufundi stadi kutolewa kote nchini.