MADATARI WALIOFELI MITIHANI WAUNDIWA TUME
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
Serikali imeunda tume kuchunguza madai ya madaktari watarajali waliofeli mitihani ya Baraza la Madaktari la Tanganyika (MCT).
Tume hiyo ya wajumbe 13 itachunguza malalamiko ya madaktari watarajali juu ya mitihani ya usajili kabla na baada ya utarajali inayotolewa na MCT.
MCT ilianza kuendesha mitihani hiyo mwaka 2020 baada ya kuanza kutumika kwa sheria mpya ya madaktari, madakrati wa meno na wataalam wa afya shirikishi sura 152 ya mwaka 2017 na kanuni zake za mwaka 2018.
Akizungumza leo Agosti 14, 2023 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema mwenendo wa ufaulu wa mitihani hiyo tangu Desemba 2020 hadi Desemba 2022 ni kati ya asilimia 68 hadi 69 lakini mtihani wa Machi 2023 ni asilimia 42 ya watahiniwa 640 ndio walifaulu.
“Niwasihi madaktari tarajali wawe na subira katika kipindi hiki ambacho kamati itakuwa inafanya uchunguzi, pale watakapohitajika kutoa maelezo mbele ya kamati watoe ushirikiano unaostahili…wizara itasimamia haki na ustawi wa taaluma ya madaktari nchini,” amesema Ummy.
Amesema kamati hiyo ya wataalam itakayofanya kazi kwa mwezi mmoja itaongozwa na Mganga Mkuu wa Serikali mstaafu ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, Profesa Muhammad Bakari na Katibu, Profesa Kisali Pallangyo (Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya Mstaafu).
Vilevile wamo Dk. Bryceson Kiwelu (Bingwa wa Upasuaji Mifupa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke), Dk. Emmanuel Gambi (Mtarajali na Kiongozi wa Watarajali Morogoro), Dk. Salvatory Kalabamu (Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Hubert Kairuki), Dk. Kennedy Hosea (Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia), Wakili Belinda Molel (Wakili, Shule ya Sheria Tanzania) na Dk. Telemu Kassile (Mkurugenzi wa Ithibati Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania).
Waziri Ummy amesema mchanganyiko wa wataalam katika kamati hiyo umelenga kutoa nafasi katika nafasi katika maeneo mbalimbali yaliyoonekana kutokuwa na ufaulu mzuri katika mitihani iliyopita.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wengine ni Dk. Alicia Massenga (Bingwa wa Upasuaji Bugando) na Dk. Kondo Chilonga (Bingwa wa Upasuaji Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC), Dk. Matlida Ngarina (Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Wanawake Muhimbili na Kiongozi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Ujauzito), Dk. Haika Maliki (Bingwa wa Watoto Lugalo na Katibu Msaidizi wa Chama cha Madaktari Tanzania) na Dk. Kamran Hameed (Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Hospitali ya Aga Khan).