CHUO CHA MAJI CHAANZISHA KOZI MPYA KUPATA WATAALAMU WABOBEZI
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, akizungumza wakati wizara hiyo ilipokuwa ikiwasilisha utekelezaji wa shughuli za chuo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Chuo cha Maji kimeanzisha Shahada mbili za Uzamili ili kuendelea kuzalisha wataalam wabobezi zaidi.
Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1974 kama kitengo ndani ya Wizara ya Maji ambapo kimechangia kuzalisha rasilimali watu inayotumika katika sekta ya maji hapa nchini na nje ya nchi.
Akizungumza Agosti 18, 2023 Mkuu wa Chuo cha Maji, Dk. Adam Karia, shahada hizo zitaanza kutolewa mwaka 2023/24.
Mkuu huyo wa chuo alikuwa akizungumza wakati Wizara ya Maji ilipokuwa ikiwasilisha utekelezaji wa shughuli za chuo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira.
"Chuo kimekuwa na mafanikio anuwai ikiwemo ongezeko la watahiniwa pamoja na machapisho ya tafiti mbalimbali ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika kukuza uchumi na kutoa majibu ya changamoto mbalimbali katika jamii," amesema Dk. Karia.
Amezitaja shahada hizo kuwa ni Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Rasilimali Maji na Huduma (Master Degree in Water Resources and Utility Management) na Shahada ya Uzamili ya Uhandisi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (Master Degree in Water Supply and Sanitation Engineering).
Aidha amesema katika kipindi cha miaka miwili 2021/22 hadi 2022/23), chuo kimedahili wanafunzi 1,727 katika ngazi ya shahada na 3,360 kwa ngazi ya stashahada.
Amesema mwaka 2021/22, chuo kilitoa wahitimu 133 wa ngazi ya shahada, 269 wa stashahada na 62 wa cheti.
"Wataalamu hawa pamoja na wengine ambao wamekuwa wakizalishwa na chuo hiki wamekuwa msaada mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji na sekta nyingine mtambuka," amesema.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jackson Kiswaga, amesema Wizara ya Maji imekuwa sikivu katika kufanyia kazi maoni na maelekezo mbalimbali hivyo imeweza kupata mafanikio ikiwamo maendeleo makubwa katika Chuo cha Maji.
Ameitaka wizara hiyo kuhakikisha watumishi wa sekta ya maji wanaendelea na utaratibu huo ili kuleta mabadiliko chanya kwa Watanzania.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameihakikishia kamati hiyo kuendelea kusimamia maagizo yote yanayotolewa ili chuo kiwe mfano bora katika vyuo barani Afrika.