RC CHALAMILA AKUTANA NA WAFANYABISHARA SOKO LA MCHIKICHINI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 17, 2023 amekutana na wafanyabishara wadogo katika Soko la Mchikichini Ilala Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akizungumza na wafanyabishara hao amepokea Changamoto ya choo na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji kulipatia ufumbuzi suala hilo mara moja.
Aidha ametoa onyo kali kwa wafanyabishara wasio waaminifu ambao huunguza masoko kwa sababu zao binafsi amelipongeza jeshi la polisi kwa kushirikiana na ulinzi shirikishi kubaini mtu aliyetaka kuchoma moto soko hilo huku akiwataka wafanyabishara hao kuwa walinzi namba moja.
Lakini pia RC Chalamila amesema amekuja Kujitambulisha kwa wafanyabishara hao na kuwasisitiza kuwa biashara ndio msingi wa maisha yao, "amekemea watu wanaoleta chokochoko na kuhatarisha amani, Dar es Salaam sio mahali pake" Alisema RC Chalamila
Hata hivyo wafanyabishara hao walionyesha kutamani kuendelea kutoa malalamiko yao kwa Mhe Mkuu wa Mkoa ndipo akawaahidi kurudi tena katika soko hilo kusikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi.
Kwa Upande wa kamanda wa kanda maalum Muliro Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi limeimarisha mifumo ya kiitelijensia ya kubaini watu waovu, hivyo wafanyabishara waendelea kufanya biashara ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla lengo la jeshi hilo ni kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara saa 24.


