KINANA: RAIS SAMIA HANA NIA YA KUUZA BANDARI
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mkendo Musoma Mjini, mkoani Mara.
Na Mwandishi Wetu, Mara
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amesema Rais Samia na serikali anayoingoza haiwezi kuuza Bandari ya Dar es Salaam huku akihoji afanye hivyo kwa masilahi gani.
Kinana ameyasema hayo Julai 26, 2023 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mkendo Musoma Mjini, mkoani Mara.
“Nataka niwahakikishie msiamini kwamba Rais aliyekula kiapo eti atafanya jambo ambalo halina masilahi na nchi. Haiwezi kutokea, Rais ambaye tangu amechukua usukani amefanya mambo mengi mazuri, kwa nini aende kuuza bandari, sababu ni ipi?
“Ili apate nini, ili iweje na ukisikiliza huu mjadala usikilizeni kwa makini na mmeshausikiliza, wote tunaoutetea, wanaopinga pamoja na wanaokosoa hakuna anayesema kwamba kusiwe na uwekezaji hata mmoja, wote wanakubali kwamba kuna haja ya kuwekeza na lengo ni moja tu kuongeza ufanisi na kuongeza mapato.
“Serikali imesema tunakwenda kufanya kazi hii kwa nia njema ya kuongeza ufanisi, kuongeza mapato tuweze kufanya shughuli nyingi zaidi za maendeleo. Wamejitokeza watu wameanza kuhoji, wako wanaohoji kwa nia njema ya kujenga ya uzalendo, hatuwezi kusema kila anayehoji anania mbaya,” amesema Kinana.