WAZIRI KOMBO AWASILISHA UJUMBE WA RAIS SAMIA KWA MUSEVENI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni Entebbe, Uganda.Ujumbe huo umewasilishwa Mei 13,2025 ambapo Waziri Kombo aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Kombo ametembelea majengo ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda yakijumuisha makazi ya awali ya Balozi yaliyopo Kololo.
Aidha Waziri Kombo alihitimisha ziara yake kwa kufanya kikao kazi na watumishi wa ubalozi wakiongozwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paul Simuli, ambapo aliweka mkazo katika masuala muhimu ikiwa ni pamoja na utendaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za Serikali, pamoja na kuibua fursa nyingi zilizopo kati ya Tanzania na Uganda.

