RAIS SAMIA, UONGOZI KKKT WAJADILI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, Ikulu jijini Dar es Salaam Aprili 11,2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu hususan wenye changamoto ya afya ya akili. 

Viongozi hao wa kanisa wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwa Kanisa hilo. Aidha, kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalumu hususan wenye changamoto ya akili, Serikali imeahidi kushirikiana na kanisa ili kujenga Kituo kikubwa zaidi watoto wengi waweze kupata huduma hiyo.


Powered by Blogger.