MAKALLA AANZA ZIARA MKOA WA LINDI

*Akagua barabara na madaraja Somanga

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amewasili mkoani Lindi leo Aprili 10,2025 kwa ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Awali baada ya kuwasili mkuani humo alipita katika Kata ya Somanga Mtama iliyopo katika Jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi kwa ajili ya kusalimia wananchi wa eneo hilo.

Alitembelea katika daraja la Somanga Mtama ambalo lilikatika na kusababisha kupotea kwa mawasiliano katika barabara ya Dar es salaam-Lindi na kuangalia hali inavyoendelea katika daraja hilo.Makalla alimpongeza Waziri Ulega kwa weledi mkubwa aliouonyesha kwa kuweza kurudisha mawasiliano hayo kwa muda mfupi na kumtaka aendelee kuwa mkali pale uzembe unapotendeka kwani anachokifanya ni kwa masilahi ya CCM kwa sababu wana dhamana kwa wananchi.

Zaidi ya Sh bilioni 100 zimetolewa kukamilisha ujenzi wa madaraja hayo, hivyo amemsisitiza Waziri Ulega kuhakikisha anasimamia wakandarasi madaraja hayo yajengwe kwa ubora na kwa hadhi inayostahili kwani fedha zipo za kutosha.

CPA Makalla anatarajiwa kufanya mkutano wake hadhara na kuzungumza na wananchi katika eneo la Kilwa Masoko.


Powered by Blogger.