DKT. BITEKO AWASILI MKOANI IRINGA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Aprili 26, amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku moja. 

Katika Uwanja wa Ndege wa Nduli, Dkt. Biteko amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Iringa, Peter Serukamba

Akiwa mkoani humo anatarajiwa kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule, Romanus Elamu Mihali, kuwa Askofu wa Jimbo la Kitume la Iringa.


Powered by Blogger.