MBUNGE MTEMVU AJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGAKURA

Na Mwandishi Wetu, The Page

Mbunge wa Jimbo la Kibamba wilayani Ubungo, Issa Mtemvu amejitokeza katika Kituo cha Kibwegere Shule, Mtaa wa Kibwegere Kata ya Kibamba mkoani Dar es Salaam kŵa ajili ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpigakura.

Mbunge Mtemvu amefanya hivyo wakati huu ambapo zoezi hilo lipo katika Mkoa wa Dar es Salaam ili aweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Hatua hiyo inakwenda aambamba na kuandikisha wapigakura wapya lakini inalenga kuboresha pia taarifa za wapigakura wa zamani wakiwemo wale waliopoteza kadi zao.Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, uandikishaji huo utafanyika kwa siku saba umeanza Machi 17 na utakamilika Machi 23, 2025.

Amesema uandikishaji huo unawahusu waliotimiza miaka 18 pia wale waliopoteza kadi zao ama kuharibika watapatiwa nyingine.



Powered by Blogger.