KAMATI YA BUNGE PAC YAKAGUA MIRADI YA KILIMO YA UMWAGILIAJI ARUSHA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Japhet Hasunga imetembelea na kukagua miradi miwili ya umwagiliaji mkoani Arusha.
Miradi hiyo iliyotembelewa Machi 23,2025 ni ule unatokelelezwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) wa ujenzi wa hekta 800 za umwagiliaji katika shamba la mbegu la Kilimo na Msimba awamu ya pili katika eneo la Ngaramtoni, Arusha.
Mradi mwingine ni ule unatokelelezwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) wa ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji katika Kituo cha Utafiti cha Seliani, Arusha.
Ziara hiyo ya Kamati ni sehemu ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.


