KAGAME, MUSEVENI WAWASILI TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA EAC NA SADC

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amempokea Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Paul Kagame, ambaye amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika jijini Dar es Salaam Februari 8,2025.


Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, amempokea Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ambaye amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika jijini Dar es Salaam Februari 8,2025.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amempokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ambaye amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025.

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Said Mshana, amempokea Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, aliyewasili nchini Februari 8, 2025 kuuwakilisha Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Said Mshana, amempokea Waziri wa Ulinzi wa Madagascar, Luteni Jenerali Sahivelo Lala Monja Delphin, aliyewasili nchini Februari 8,2025 kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Said Mshana, amempokea Waziri Mkuu wa DRC, Judith Suminwa, aliyewasili nchini Februari 8,2025 kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).






Powered by Blogger.