AIRTEL YAWAZAWADIA WATEJA PROMOSHENI SANTA MIZAWADI

Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando, akizungumza wakati wa droo ya promosheni ya Santa Mizawadi makao makuu ya kampuni hiyo, Dar es Salaam.

Na Nora Damian, The Page

Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania imeanza kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Santa Mizawadi katika msimu huu wa sikukuu.

Zawadi hizo zimetolewa leo Desemba 24,2024 katika droo iliyochezeshwa makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Katika droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha washindi wamejishindia bodaboda, rota, simu janja, luninga ya nchi 55 na fedha taslim Sh milioni moja.

Washindi na zawadi zao kwenye mabano ni Josephine Mgagula mkazi wa Nzega mkoani Tabora aliyejishindi rota na bando la Sh 110,000 kwa mwezi mzima, Omary Ramadhani wa Shinyanga (simu janja), Fatma Mwachoyo wa Dar es Salaam (pikipiki ya miguu miwili), Halima Kimaro wa Shinyanga (luninga) na Andrea Kyoma wa Ifakara Morogoro (Sh milioni moja).Akizungumza wakati wa droo hiyo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano, Jackson Mmbando, amesema promosheni hiyo ni ya wazi kwa wateja wote nchini na kuwataka kuendelea kutumia huduma za Airtel.

Naye Fatma aliyejishindia bodaboda amesema; "Nawashukuru sana Airtel kwa kuandaa promosheni hii na kunizawadia bodaboda, nawashauri watu wengine watumie mtandao wa Airtel.

Kampuni hiyo imesisitiza kuwa washindi wote watapigiwa simu kupitia namba maalumu ya huduma kwa wateja 100 na kuwataka kuwa makini kuepuka matapeli.




Powered by Blogger.