4R ZA RAIS SAMIA: WAZIRI LUKUVI ATUMA SALAMU KWA VYAMA VYA SIASA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Chama cha UPDP, Dar es Salaam.

Na Nora Damian, The Page

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi amevitaka vyama vya siasa amevitaka vyama vya siasa kushindana kwa hoja kuelekea Uchaguzi wa Serikali Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Lukuvi ametoa kauli hiyo Oktoba 7,2024 baada ya kutembelea vyama vya siasa vya CHAUMA, ACT Wazalendo UPDP na CCK kwa lengo la kueneza falsafa ya Rais Samia ya R4 na kuwa karibu na viongozi wa vyama vya siasa.

“Tunajenga bondi na kuimarisha falsafa ya mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya R4 ambayo inataka tuwe na ushirikiano wa karibu na vyama vya siasa ambao ndiyo wadau wa siasa wa nchi hii, wakati umefika wa kushindana kwa hoja, ni wajibu wetu kudumisha amani na upendo.“Huu ndiyo wakati wa kushindanisha sera zetu kwa hoja na baada ya hapo tukishapata matokeo tuwaachie waliochaguliwa watekeleze wajibu wao kwa miaka mitano kwa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani,” amesema Lukuvi. 

Amesema anapeleka salamu za upendo kwenye vyama na kuwahimiza juu ya ushiriki wao katika uchaguzi na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wakazi ili wapate fursa ya kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi huo.




Powered by Blogger.