MWENDA BOSI MPYA TRA, JAFO APELEKWA VIWANDA

Rais Samia Suluhu Hassan.

Na Mwandishi Wetu, The Page


Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk. Selemani Jaffo kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Dk. Ashatu Kijaji.

Dk. Kijaji amehamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) nafasi aliyokuwa akiishikilia Dk. Jaffo.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, wengine walioteuliwa ni Yusuf Mwenda kuwa Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya uteuzi huo Mwenda alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB). Anachukua nafasi ya Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Ofisi ya Rais Ikulu.



Powered by Blogger.