KILICHOSABABISHA BRELA KUPATA TUZO SABASABA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa, akiwa na tuzo waliyokabidhiwa baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa jumla wa banda bora kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). Kulia ni Rais Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi.
Na Nora Damian, The Page
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa amesema utendaji kazi wenye weledi umewezesha kupata tuzo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.
Brela imepata tuzo ya mshindi wa tatu wa jumla wa banda bora.
Akizungumza Julai 3,2024 na Waandishi wa habari katika banda la Brela lililopo kwenye maonesho hayo, Nyaisa amesema watahakikisha tuzo hiyo inaendelea kuakisi utendaji wao katika shughuli za kila siku.
“Tuzo hii ni uthibitisho kwamba Brela tumetoka wapi, tuko wapi na tunakoelekea ni wapi, mwaka jana nafasi hii hatukuipata, tulifanikiwa kuwa washindi wa pili katika kipengele cha taasisi zinazofanya kazi kama za Brela, tunataka tuone tuzo tuliyoipata mwaka huu inaakisi pia utendaji kazi wetu katika shughuli zetu za kila siku.
“Kitu ambacho ni tofauti tumekifanya hadi kupata tuzo; siku hizi tunakuja kwenye maonesho kufanya kazi, watendaji wote ofisini wanakuja kufanya kazi. Tunaonesha na tunafanya kazi, mtu anayetaka leseni ataipata hapa, anayetaka kusajili kampuni atasajiliwa na atapewa cheti.
“Mambo yetu mengi tunayafanya kupitia kwenye mifumo ya kidijitali, tuko tofauti na mabanda mengine ya wenzetu, pia morali ya wafanyakazi ni kubwa…unaweza kuonekana unafanya vizuri lakini ni lazima uwawezeshe wafanyakazi ili wawe na ‘confidence’ na kazi wanayoifanya,” amesema Nyaisa.

Mtendaji huyo wa Brela amesema utayari wa Serikali na mamlaka zake pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini kumewezesha kuongezeka kwa idadi ya biashara zinazoanzishwa.
Amesema katika maonesho hayo shughuli mbalimbali kama zinafanyika kama vile utoaji leseni za biashara, usajili wa kampuni, usajili wa alama za biashara na nyingine na kuwakaribisha Watanzania kutembelea banda la Brela.