MSHINDI POOL TABLE KIVULE KUSAKWA JUMAMOSI


Na Mwandishi Wetu, The Page


Timu nne zinatarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kutafuta mshindi wa mchezo wa Pool Table Jumamosi wiki hii.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo, Kivule Garden, mashindano yataanza saa 10:00 jioni na mshindi atajinyakulia zawadi nono pamoja na kreti tano za bia.

Akizungumzia mpambano huo Katibu wa Kivule Garden, Mudy Madati, amesema timu zilizoingia kwenye mashindano ni nne.
Amezitaja timu hizo kuwa ni Dodoma Veteran, Kivule Garden, Marafiki Pub na Kivule Veteran.

"Dodoma Veteran watacheza na Kivule Garden na Marafiki Pub watacheza na Kivule Veteran, mshindi atapata kreti za bia za kutosha," amesema Mudy.

Timu ya Marafiki Pub kupitia mlezi wao Kulwa Mzee, amesema wamepokea mwaliko huo wa kujenga ushirikiano kwa furaha na wameahidi kubeba ushindi.

Akizungumzia malengo mengine ya mashindano hayo, Shangazi Sandra Sudi, amesema yanalenga kujenga ushirikiano, kufanya biashara na kukuza vipaji vya vijana.
Powered by Blogger.