SERA YA MILIKI BUNIFU MBIONI KUKAMILIKA
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinyjuma (Wapili kushoto), akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wabunifu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Miliki Bunifu, Dar es Salaam.
Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha sera ya taifa ya miliki bunifu itakayotoa mwongozo thabiti katika kusimamia masuala hayo.
Akizungumza leo Mei 9,2024 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Miliki Bunifu, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinyjuma, ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, amesema maendeleo yoyote yanategemea miliki bunifu ndiyo maana wanaendelea kuboresha sheria mbalimbali ili kuendana na hali ya sasa.
“Serikali itaendelea kuziwezesha taasisi zinazosimamia miliki bunifu ili kuendana na kaulimbiu ya mwaka huu kwa kuwa bila miliki bunifu hakuna maendeleo yoyote ya kiuchumi na kijamii. Yote tunayoyafanya lakini tujielekeze kuhakikisha miliki bunifu inatambuliwa wabunifu waweze kunufaika na bunifu walizonazo,” amesema Mwinyjuma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Geofrey Nyaisa, amesema bado kuna changamoto ya uelewa wa masuala ya miliki bunifu na kwamba wameendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyuo, wafanyabiashara na wajasiriamali ili kuhakikisha bunifu zinalindwa na kutumika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kwa mujibu wa Nyaisa, mwaka 2023/2024 wametoa elimu katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM), Chuo Kikuu za Mzumbe, vyuo vya Veta na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO). Pia wametoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Geita, Njombe.
Brela pia wanatoa ufadhili wa masomo ya shahada ya uzamili katika miliki bunifu kwa kushirikiana na Shirika la Miliki Bunifu Kanda ya Afrika ili kuongeza wataalam katika eneo na mpaka sasa wanafunzi 13 wamenufaika.
Katika hafla hiyo Brela imeingia makubaliano ya ushirikiano na TIA, Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) ili kuimarisha shughuli za miliki bunifu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Geofrey Nyaisa, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Miliki Bunifu, Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, amesema makubaliano hayo yataongeza tija na kuimarisha usalama wa afya ya binadamu na mazingira.
“Tulibaini changamoto mifumo ilikuwa haisomani, kila taasisi ilikuwa inafanya kazi kivyake hivyo, makubaliano haya yatasaidia kutatua changamoto na mifumo itasomana. Tutaandaa mafunzo ya pamoja kuhakikisha wafanyabiashara wanaosajili viuatilifu wawe tayari wamejisajili Brela,” amesema Profesa Ndunguru.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy, ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira yanayochochea matumizi ya shughuli za ubunifu nchini kwani zina mchango mkubwa katika kutatua changamoto za sekta mbalimbali.
Siku ya Miliki Bunifu huadhimisha Aprili 26 kila mwaka lakini imeadhimishwa leo kwa sababu ya sherehe za miaka 60 ya Muungano. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema ‘Miliki ubunifu na malengo ya maendeleo endelevu; kujenga mustakabali wa pamoja kwa kutumia ubunifu’.
Na Nora Damian, The Page