SHIRIKA LAIANGUKIA SERIKALI BIMA YA AFYA KWA WATOTO
Mwenyekiti wa Shirika la Diana Women Empowerment, Farida Khakoo.
Shirika lisilo la kiserikali linalohudumia yatima, wajane, wenye ulemavu na wazee (Diana Women Empowerment) limeiomba Serikali kuangalia upya utaratibu wa utoaji bima ya afya kwa watoto ili kuwawezesha kupata matibabu kirahisi.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ulibadili utaratibu kutoka ule wa awali wa kuwasajili watoto kwa bima ya afya ya Toto Afya Kadi na kuwasajili kupitia vifurushi au shule wanazosoma.
Akizungumza Februari 14,2024 na waandishi wa habari Mwenyekiti wa shirika hilo, Farida Khakoo,
amesema utaratibu huo utasababisha watoto wengi kukosa huduma hiyo.
"Watoto wengi tunaowahudumia wako chini ya miaka mitano hawajaanza shule na wanatoka katika familia duni.
"Wazazi wao hawana uwezo wanatutegemea sisi, wanashindwa kugharamia matibabu na watoto wengi wanatumia dawa kila siku kwahiyo watashindwa kupata huduma," amesema Farida.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo mwaka 2022 walisaidia watoto 112 kupata huduma ya bima ya afya lakini mwaka 2023 waliopata huduma hiyo ni 12 tu.
Amesema pia watoto wengi wanaowahudumia wana ulemavu na wanaishi kwenye mazingira magumu na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia.
"Tunashirikiana na wafadhili na watu wengine wenye mapenzi mema kusaidia watoto hawa lakini uhitaji ni mkubwa hivyo, tunawaomba Watanzana na wadau wengine wajitokeze kuwasaidia,” amesema.
Mwaka 2022 shirika hilo pia lilitoa msaada wa viti mwendo na kadi za bima ya afya kwa watoto wenye ulemavu wanaosoma Shule za Msingi Ukombozi na Majimatitu kitengo cha wenye ulemavu, wanaolelewa majumbani na watoto yatima.
Shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1995 linahudumia yatima, wajane, wenye ulemavu na wazee katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga kwa kuwapatia elimu, bima za afya, chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Na Nora Damian, Dar es Salaam