MRADI WA MAJI SAME - MWANGA - KOROGWE SASA ASILIMIA 83
Na Mwandishi Wetu
Mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe unaendelea kutekelezwa kwa kasi na sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 83.5
Kiongozi msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Abbas Musilim, amesema kwa Oktoba 2023 mambo yaliyofanyiwa kazi ni pamoja na ujenzi wa kituo cha umeme uliofika asilimia 55 na kazi za kihandisi asilimia 66.
Kazi zingine zilizofanyika ni ulazaji wa bomba kutoka eneo la Kiverenge hadi Vudoi Mwanga ambapo zimelazwa kilomita 15.8 bado kilomita 5.2.
"Ulazaji wa bomba kutoka Kisangara kwenda Kiverenge umefanyika kwa kilomita 6.1 bado kilomita 7.4," amesema.
Aidha amesema ulazaji wa bomba kutoka Kiverenge kwenda Same umefanyika kwa kilomita 15.3 na kwamba bado kilomita 2.3.
Kwa mujibu wa mhandisi huyo, ujenzi wa kituo cha umeme cha Kisangara, sehemu ya kuweka transforma na miundombinu ya umeme umekamilika, inasubiriwa transforma Desemba 2023.
Kwa mujibu wa mhandisi huyo, ujenzi wa kituo cha umeme cha Kisangara, sehemu ya kuweka transforma na miundombinu ya umeme umekamilika, inasubiriwa transforma Desemba 2023.